breaking news New
Zamu ya Paul Scholes baada ya Neville na Henry kuchemka

Zamu ya Paul Scholes baada ya Neville na Henry kuchemka

Kiungo wa zamani wa Club ya Man United Paul Scholes amepewa shavu la kuwa kocha mkuu wa timu ya Oldham Athletic kwa mkataba wa mwaka mmoja, Scholes mwenye umri wa miaka 44 ambaye amezoeleka kuonekana kama mchambuzi wa soka wa soka ametambulishwa leo kama kocha.

Hiyo itakuwa fursa mpya kwa Paul Scholes kuonesha uwezo wake, kwani wengi wameanza kumnanga mitandaoni kuwa alikuwa anakosoa wenzake sasa, ni wakati wake wa kuonesha uwezo mkubwa kama ambavyo alikuwa anaonesha uwezo mkubwa katika kuchambua, huku wakitolewa mifano wakina Garry Neville na Thierry Henry kuchemka katika kazi za ukocha.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Paul Scholes alikuwa staa wa Man United aliyefanya vizuri katika club toka alipokuwa kwenye Academy ya Man United kuanzia mwaka 1991 hadi 1993, baada ya hapo akaanza kuingia kwenye kikosi cha wakubwa cha Man United alichodumu nacho hadi mwaka 2013 alipoamua kustaafu.

Leave a Comment