Yanga yazidi kujiimarisha kileleni

Yanga yazidi kujiimarisha kileleni

TIMU ya Yanga SC imezinduka baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Ushindi huo wa kwanza ndani ya mechi nne za Ligi Kuu ikitoka kufungwa 1-0 na Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na sare mfululizo, 1-1 na Coastal Union hapo hapo Mkwakwani na 0-0 na Singida United Uwanja wa Namfua, Singida unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 58 baada ya kucheza mechi 23.

Na hiyo inamaanisha Yanga SC sasa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi 10 zaidi ya Azam FC wanaofuatia katika nafasi ya pili, ingawa wana mechi mbili mkononi, wakati mabingwa watetezi, Simba SC ni wa tatu kwa pointi zao 36 za mechi 15.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Heri Sasii aliyesaidiwa na Soud Lila na Shaffid Mohammed, bao pekee la Yanga SC limefungwa na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah, maarufu kwa jina la utani Fei Toto dakika ya 26 kwa shuti la mguu wa kulia akimalizia krosi ya beki Gardiel Michael kutoka kushoto

Leave a Comment