Yanga yapata pigo jingine

Yanga yapata pigo jingine

Uongozi wa Yanga umelazimika kumrudisha haraka jijini Dar es Salaam kiungo wake Thabani Kamusoko.

Kamusoko amerudishwa kwa ajili ya Matibabu kufuatia kuchanika nyama za paja wakati wa mazoezi ya jana yaliyofanyika Popatlal Secondary jijini Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hivyo zinasema Kamusoko alishindwa kumaliza mazoezi ya jana jioni na baada ya uchunguzi.

Daktari wa timu, Edward Bavu aliamuru kiungo huyo asafirishwe kurejea Dar haraka.

Na wakati huo kikosi cha Yanga kitakuwa kinacheza kesho na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara jijini Tanga.

Leave a Comment