breaking news New
Uimarishwaji wa soka la vijana

Uimarishwaji wa soka la vijana

Na

Timotheo S John

Mchezo wa soka ni moja kati ya mchezo unaoongozwa na kanuni pamoja na sheria Kwa ajili
ya kuweza kufanya kuwa mchezo wa usawa na haki.

Hakuna shaka maendeleo makubwa ya Soka yanategemea zaidi katika msingi wa kukuza soka
la Vijana kuanzia umri wa miaka 5 hadi miaka 20.

Kanuni ya soka imeeleza kuwa ni vyema walau Kwa kila timu ya mpira kuwa na academyake ya soka Kwa lengo la kusaidia uimarishwaji wa soka la Vijana kuanzia katika umri Mdogo mpaka kuweza kufikia katika umri ambao wataweza kuitumikiaklabu husika.

Kanuni hiyo inapendekeza hivyo kwa malengo makuu mawili moja Ni kutaka kuweza kupunguza utegemezi wa vilabu kufanya usajili wa wachezaji wapya kwa 100 katika dirisha la usajili ili klabu husika iweze kuepukana na Gharama husika katika klabu.Lakini pia inakuwa ni rahisi sana kwa klabu kuweza kupata mapato kulingana na mauzo ya wachezaji husika katika viloabu vingine au wachezaji haokutolewa kwa mkopo.

Sababu ya pili ni Kuwa kwa kuwa katika vilabu vingi vinaishi kwa kutegemea Falsafa ya klabu husika hapa nazungumzia nchi zilizoendelea kama Uholanzi na Ajax katika miaka ya nyuma walifanikiwa kulinda Falsafa yao kutokana na kutegemea wachezaji kutoka katika Academy.

Tutazame uhusiano uliopo kati ya kanuni hiyo tajwa na uhalisia wa soka kwa hapa Tanzania,Utagundua kuwa Kwa hapa Tanzania bado hiyo kanuni haijawa na matunda makubwa katika soka ndio maana vilabu vingi vimewekeza zaidi katika kununua wachezaji kutoka nje ya nchi au wale ambao tayari wameishakuwa wakomavu katika mchezo wa soka.

Baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Tanzania Bara timu ya Singida United dhidi wametangaza kufanya usaili kwa ajili ya wachezaj mbalimbali ambao wapo mtaani lakini wana uwezo wa kucheza soka ,Ndio ni jambo jema lakini wao wakiwa kama klabu lazima wakubali kuwa inakuwa ngumu
kuwa na Falsafa husika ambayo itaweza kutambulisha klabu yao na kufanya luwe na utofauti kati ya dhidi ya vilabu vingine.

Singida United walipaswa kuwa na Academy yao tangu mwanzo ambayo itakuwa inauwezo wa kuwakuza wachezaji ambao inaweza kuwatumia Kwa baadae katika klabu jambo ambalo litapelekea zaidi kupunguza gharama za usajili. Kwani wao watakuwa wanawatumia wachezaji ambao wamewazalisha wenyewe na wanakuwa na mioyo ya kizalendo katika klabu. Huenda Singida wakawa wanaonekana kuwa wamechelewa katika hilo hapana bado wanaweza kama wakiaamua kuwekeza kwani soka la kisasa linaanzia katika kukuza soka laVijana.

Kwani bahati nzuri ni Kuwa mkiwa na academy kwa kuwa inakuwa na Falsafa na misingi ambayo mnaiamini inakuwa ni rahisi kwa timu kuweza kutafuta mwalimu ambaye ataweza kuwatumia Vijana ambao ni zao la timu kuliko kila mwalimu akija anaanza kufikiri kuhusu usajili mpya wa wachezaji.

Mbali zaidi na kukuza vijana klabu husika inanufaika kupitia mauzo Wachezaji husika katika klabu ambayo itaonyesha nia ya kumhitaji mchezaji wao ,Pesa ambayo Iapatikana wanaweza kuwekeza katika kukuza Vijana wengine zaidi katika klabu.

UMUHIMU WA KUKUZA SOKA LA VIJANA

1.Inampa faida mwalimu kuweza kupandikiza mbinu na imani za timu husika kwa wachezajiwakiwa katika umri mdogo.

2.Kuwafundisha wachezaji nidhamu ,Kuna tofauti kubwa ya kinidhamu kati ya mchezaji ambaye kacheza soka la academy na yule mchezaji wa ambaye hajakulia katia kituo cha uimarishwaji wa vipaji vya watoto.

CHANGAMOTO ZA SOKA LETU KATIKA KUKUZA SOKA LA
VIJANA

1.changamoto ya Miundombinu.

Kuna uhaba mkubwa wa miundombinu ya kutumika katika kukuza Vijana wakiwa katika umri mdogo ,Ukitazama vilabu Vinci having viwanja vyake zaidi ya kutegemea viwanja vya wadhamini.

2.Ukata katika klabu husika.

Sio rahisi kuweza kuwa na Academy ya soka kutokana na changamoto ya Ukata kwa hapa Tanzania kuna vituo vichache kama Alliance Schools Academy ,Mandozi Sports Academy ya Simiyu inayomilikiwa na Armando Phili ,Walau katika ligi kuu Azam FC na Mtibwa Sugar wamefanikiwa katika hilo.

Leave a Comment