Ufalme wa Sergio Aguero EPL

Ufalme wa Sergio Aguero EPL

Idadi ya magoli aliyofunga dhidi ya chelsea yamemfanya avunje rekodi ya Eric Brook na Timmy Johnson ya magoli 158 katika klabu ya City ambapo Sergio Kun Aguero amefikisha magoli 160.

Aguero sasa anashikilia rekodi ya kuwa mmoja kati ya wacheza 6 waliohusika katika magoli 200 ndani ya klabu moja, akiwa pamoja na Wayne Rooney, Ryan Giggs, Thierry Henry, Frank Lampard, na Steven Gerrard.

Aguero msimu huu amebakiza magoli matatu kufikia rekodi yake ya kufunga magoli 20+ ndani ya misimu mitano mfululizo.

2015 [Mechi 33 Magoli 26]
2016 [Mechi 30 Magoli 24]
2017 [Mechi 31 Magoli 20]
2018 [Mechi 25 Magoli 21]
2019 [Mechi 23 Magoli 17]

Rekodi hiyo pia anafungana na Hary Kane

2015 [Mechi 34 Magoli 24]
2016 [Mechi 38 magoli 25]
2017 [Mechi 30 Magoli 29]
2018 [Mechi 37 Magoli 30]
2019 [Mechi 22 Magoli 14]

Kwa sasa ndiye kinara wa ufungaji mabao dhidi ya vilabu 6 bora.

Aguero – Magoli 43
Vardy – Magoli – 29
Rooney – Magoli – 23
Kane – Magoli – 21

Aguero sasa anaingia kwenye orodha ya wachezaji wanaongoza kwa kufunga Hat trick nyingi :

11 Sergio Aguero (Mechi – 229)
11 Alan Shearer (Mechi – 441)
9 Robbie Fowler (Mechi -379)
8 Thierry Henry (Mechi -258 )
8 Harry Kane (Mechi – 175 )
8 Michael Owen (Mechi -326)

Leave a Comment