Udhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Udhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Rais wa TFF Wallace Karia kupitia hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa TFF 2019 amesema bado wapo katika mkakati wa kutafuta mdhamini wa ligi kuu na tayari wameingia makubaliano na kampuni ya EAG Group kwa ajili ya kuwatafutia mdhamini.

Karia amesema mdhamini wa zamani wa ligi kuu kampuni ya Vodacom si kwamba iliondoka au kuacha kudhamini bali walishindwa kufikia makubaliano kuhusu udhamini mpya.

“Kuhusu udhamini wa ligi kuu tumeingia makubaliao na kampuni ya EAG kututafutia wadhamini, watu wanashindwa kuelewa kwamba si kwamba Vodacom wameondoka kuidhamini ligi yetu bali tumeshimdwa kufikia makubaliano ambayo naamini kama tungeyakubali kila mmoja wenu angetuona hatuna akili.”

“Ili uthaminiwe nilazima ujithamini kwanza wewe, na sisi tumemua kujithamini wenyewe, hatutaki kuwa na mdhamini tu eti kwasbaabu ni fulani.”

Ligi kuu msimu huu 2018/19 imeanza bila kuwa na mdhamini hadi sasa huku baadhi ya timu zikiwa zimeshacheza mechi 24 za ligi!

Leave a Comment