U20 Afrika : Mali yashinda ubingwa wa Afrika

U20 Afrika : Mali yashinda ubingwa wa Afrika

Timu ya taifa ya vijana ya Mali chini ya miaka 20 imeshinda ubingwa wa Afrika baada ya kuifunga Senegal kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-2 kufuatia dakika 120 kumalizika kwa sare 1-1 kwenye mashindano yaliyokuwa yanafanyika nchini Niger.

Mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano hayo ilizikutanisha timu hizo zilizopangwa Kundi B, katika mchezo huo (ufunguzi) Mali ilifungwa 2-0.

Mashindano yamemalizika lakini timu 4 zilizofanikiwa kuingia nusu fainali (Mali, Senegal, Afrika Kusini pamoja na Nigeria) zimekata tiketi ya kuiwakilisha Afrika kwenye michuano ya dunia chini ya miaka 20 ambayo itafanyika Poland.

Kama unakumbuka, Mali ilishinda ubingwa wa michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (walikuwa kundi moja na Serengeti Boys).

Kwenye ukanda wetu tuliwakilishwa na Burundi ambao waliishia hatua ya makundi ambapo wachezaji watatu walitoka ligi kuu Tanzania bara.

Leave a Comment