Tottenham Hotspur kimyakimya kwenye mbio za Ubingwa

Tottenham Hotspur kimyakimya kwenye mbio za Ubingwa

Mabao kutoka kwa Davinson Sanchez dakika ya 33, Christian Eriksen dakika ya 63 na Heung-Min Son dakika ya 90 yanaifanya Tottenham kuzidi kuisogelea Livelpool baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Leicester Uwanja wa Wembely

Hili ni bao la kwanza kwa Sanchez’s kwenye Premier League ambaye alikuwa wa kwanza kufunga katika mchezo huo.

Jamie Vardy alitokea bench kipindi cha pili na alipiga penalti iliyookolewa na Hugo Lloris dakika ya 60.

Ushindi huu unazidi kumtakatisha Meneja Mauricio Pochettino’s kwa upande wake akiwa na matumaini ya kufika kwenye tatu bora ya Premier League’s.

Tottenham inakuwa mbele zaidi kwa pointi nane ikiwaacha Manchester United baada ya kufikisha pointi 60 huku Leicester City wakibaki nafasi ya 12 wakiwa na pointi 32.

Leave a Comment