Tetesi za Soka Ulaya (deadline day)

Tetesi za Soka Ulaya (deadline day)

Winga wa zamani wa klabu ya Manchester United Nani, 32, ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Sporting Lisbon, anatazamiwa kujiunga na ligi ya soka Marekani, MLS. (beIN Sport USA, via ESPN)

Mchezaji wa Tottenham Georges-Kevin N’Koudou anafanya vipi huko Monaco kukamilisha makubaliano mkopo kwa team hiyo ya Ligue 1 (Sky Sports)

Meneja wa RB Leipzig Ralf Rangnick amethibitisha Emile Smith-Rowe anafanya vipimo kwenye club hiyo kwa makubaliano ya mkopo kutoka Arsenal (Sky Sports)

Paris St-Germain wametoa ofay a dakika za mwisho ya kutaka kumsajili kwa mkopo mchezaji wa Arsenal, Mjerumani Mesut Ozil, 30. (Metro)

PSG pia wanataka kumsajili winga wa Chelsea na Brazil Willian, 30, kwa mkopo kama mbadala wa Neymar ambaye ni majeruhi. (Mail)

West Ham wamefanya mazungumzo na Chelsea wakitaka kujua uwezekano wa kumsajili streka wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 32. (Mail)

West Ham pia wanamuwinda kiungo wa Chelsea Danny Drinkwater, 28, ili wamsajili kwa mkopo. (Talksport)

Tyrone Mings mbioni kujiunga kwa mkopo Aston Villa kutoka Bournemouth (Sky Sports)

West Ham wamekataa kitita cha pauni milioni 7 kutoka Valencia kwa usajili wa mshambuliaji wa Mexico Javier Hernandez, 30. (Sky Sports)

Leave a Comment