breaking news New
Tanzania yatwaa Cosafa mbele ya Zambia

Tanzania yatwaa Cosafa mbele ya Zambia

Timu ya wanawake ya Tanzania chini ya Umri wa miaka 20 imefanikiwa kutwaa taji la mashindano ya wanawake kwa upande wa Kusini baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Zambia 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Wolson.

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Oppa Clement dakika ya 24 na Protasia Mbunda kwenye dakika ya 87 akifunga kwa shuti kali.Ushindi huo Unaifanya Tanzania kuwa timu ya kwanza alikwa kufanikiwa kubeba taji kwenye mashindano hayo.

Mambo unayopaswa kuyafahamu kutoka kwa Tanzania hususani katika ushiriki wao kwenye mashindano hayo

1.Tanzania ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuwatoa timu wqenyeji ambaye pia alikuwa Bingwa mtetezi wa mashindano haya 2-1 ambaye alikuwa ni Afrika ya Kusini.

2.Tanzania imetoa mchezaji pekee ambaye amefanikiwa kufunga hat trick katika mashindano haya ambaye ni Aisha Khamis anayeichezea timu ya wanawake ya Alliance ya Jijini Mwanza.

3.Mfungaji bora wa Tanzania kwenye mashindano haya ni mlinzi aitwae Enekia Kasonga ambaye amefanikiwa kufunga magoli 4 katika mashindano.

4.Tanzania wameruhusu kufungwa magoli 4 pekee huku wao wakifunga jumla ya magoli 15 kwenye mashindano yote.

Leave a Comment