Tambwe Kuwakosa Wagosi wa Kaya

Tambwe Kuwakosa Wagosi wa Kaya

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Amisi Tambwe hatakuwa sehemu ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Februari 3 mwaka huu (jumapili) kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga kutokana na kuwa majeruhi.

Tambwe aliumi kwenye mchezo wa Kombe la shirikisho FA dhidi ya Biashara United ambapo katika mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa penati 5-4 na kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Mratibu wa Klabu hiyo Hafidhi Salehe amesema kuwa Timu inaendelea vizuri na leo itasafiri kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, ila Tambwe hatakuwa sehemu ya wachezaji watakao safiri kutokana na majeraha aliyonayo.

Tambwe aliumia kwenye mchezo wetu wa FA dhidi ya Biashara, ameshonwa nyuzi 3 kwenye paji la uso lakini sasa anaendelea vizuri na wachezaji wengine wanaendelea vizuri na tumefanya mazoezi kwenye viwanja vya polisi kurasini na mchana tutaanza safari ya kuelekea Tanga kwa ajili ya mchezo wetu”

- Amesema Hafidhi

Leave a Comment