Simba Sc yapindua matokeo vs Al Ahly, Js Saoura waondoka na point tatu vs As vita

Simba Sc yapindua matokeo vs Al Ahly, Js Saoura waondoka na point tatu vs As vita

Simba SC wakiwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya Al Ahly wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 65 na kujikusanyia point tatu zilizowafanya wafikishe jumla ya point 6, huku Al Ahly wakiwa wanaendelea kuongoza Kundi lao D wakiwa wamesalia na point zao 7.

Simba sc imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika pongezi kwa mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere aliye katika msimu wake wa kwanza tu Simba SC tangu awasili kutoka Gor Mahia ya Kenya.

Kagere alifunga bao hilo dakika ya 65 kwa shuti la mguu kulia akimalizia pasi ya kichwa ya Nahodha na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, John Raphael Bocco kufuatia krosi ya beki Zana Coulibaly kutoka Burkina Faso.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi nne ikipanda kwa nafasi moja hadi ya pili, nyuma ya Al Ahly wenye pointi saba

Mchezo mwingine wa kundi D JS Saoura ya Algeria anayoichezea Mtanzania, Thomas Ulimwengu imeitwanga AS Vita kwa bao 1-0 katika mchezo wa Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Ushindi huo wa Saoura iliyokuwa nyumbani Algeria, unaifanya AS Vita inakwenda kushika mkia

Kwa sasa, Ahly inaongoza kwa kuwa na pointi saba, ikifuatiwa na Simba yenye sita na Saoura ina nne wakati Vita wako mkiani na pointi 4.

Leave a Comment