breaking news New
Simba Sc wamtambia mtani wa Jadi ‘TPL’, Meddie Kagere tena

Simba Sc wamtambia mtani wa Jadi ‘TPL’, Meddie Kagere tena

Baada ya kucheza mchezo wa Club Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa club ya Simba SC na kuibuka na ushindi wa goli 1-0,

Simba ikiwa tena uwanja wa Taifa kupitia kwa yule yule Meddie Kagere imefanikiwa kuifunga Yanga kwa goli 1-0, lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 71, Meddie Kagere anaipatia ushindi Simba kwa mara ya pili mfululizo upande ule ule wwa goli, hiyo ni baada ya kuwalaza Al Ahly mapema wiki iliyoisha.

Simba walianza vizuri kipindi cha kwanza wakitawala karibu dakika 20 zote, Hata hivyo, Simba hawakuwa makini kutumia nafasi nyingi walizopata. Kuanzia dakika ya 28, walianza kuonekana kupoteza kasi waliyonayo na kuwaachia Yanga nafasi kucheza.

Mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi na beki kinda wa Yanga, Paulo Godfrey walikuwa kivutio kikubwa leo, Okwi aliyekuwa akicheza wingi ya kushoto, alikutana na Paulo ambaye alikuwa beki wa kulia na ushindani wao, uliwafanya wengi kuwatazama kwa ukaribu, Paulo ambaye amechukua namba hiyo “mkononi” mwa Juma Abdul, wa kiasi kikubwa alifanikiwa Okwi asipeleke madhara.

Yanga Wakicheza kwa sehemu kubwa katika mfumo wa 3-5-2, Yanga hawakuonesha nia ya kutafuta ushindi, zaidi ya sare au kufungwa mabao machache. Hii inathibitishwa na kikosi ambacho mwalimu Zahera, alianza nacho. Kumfanya Feisal acheze chini, badala ya katikati kwenye wale watano, kunadhihirisha ni namna gani kocha hakutaka kushambulia.

Upande mwepesi kwa Yanga kupita ulikuwa kushoto ambako Zimbwe Jr. hakucheza kwa nidhamu ya ulinzi. Zahera angemtuma Ngassa aongeze presha upande huu na kumlazimisha Zimbwe Jr. kurudi nyuma. Hii ingemlazimisha kufanya makosa zaidi ya aliyokuwa akiyafanya bila presha. Lakini Zahera alikuwa na mipango yake.

Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kilichomshinda kwenye mchezo wake ni ubunifu kwa wachezaji kwani walizidiwa maarifa na wachezaji wa Simba, Zahera amekubali kupoteza mchezo wake wa leo na kuwaweka kiporo Simba mpaka mwakani ili awatungue mabao mengi zaidi.

Mzunguko wa kwanza Simba akiwa mwenyeji alilazimisha suluhu ila leo akiwa mgeni amemfunga mtani wake Yanga bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.

Leave a Comment