breaking news New
Simba SC Mabingwa wa Ngao ya Jamii tena

Simba SC Mabingwa wa Ngao ya Jamii tena

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Simba SC leo walikuwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezom wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC ambao ndio Mabingwa wa Kombe la FA, mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa Simba SC aliendeleza ubabe kwa kutwaa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kwa kuwafunga 4-2.

Magoli ya Simba SC yalifungwa na Shibob aliyefunga mawili dakika ya 16 na 22 , Cloutus Chama dakika ya 56 na mwisho likafungwa na Francis Kahata dakika ya 83, huku magoli ya Azam FC yakifungwa na Shaban Iddi Chilunda dakika ya 13 na Frank Domayo dakika ya 78.

Kuchezwa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii huwa ni ishara ya kwenda kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2019/2020, wakati ambao Simba SC na Azam FC watakuwa wamemaliza mechi zao za marudiano za kimataifa, Ligi Kuu itaanza tarehe 23 2019.

Leave a Comment