breaking news New
Samata atikisa Ubelgiji

Samata atikisa Ubelgiji

Mtanzania Mbwana Samata ameendelea kutikisa katika ligi ya Ubelgiji ambapo jana kafanikiwa kuifungia timu yake ya KRC Genk magoli 3 yaani Hat trick walipofanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Waasland Beveren.

Hat trick hiyo inamfanya Samata kufikisha magoli 4 katika ligi hiyo kwa msimu huu lakini pia ikiwa ni Hat trick yake ya 3 akiwa na Genk baada ya kufunga hat trick mbili mwakan uliopita , Alifanikiwa kufunga dhidi ya Broendby IF kwenye mchezo wa kufuzu Europa ligi pia dhidi ya Zulte Waregem kwenye mchezo wa ligi kuu.

Ushindi huo unawafanya Genk kufikisha alama 6 wakiwa kwenye nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu .Kinara wa ligi hiyo ni Club Brugge wenye alama 10.

Leave a Comment