breaking news New
Samata atikisa michuano ya Ulaya

Samata atikisa michuano ya Ulaya

Mtanzania Mbwana Ally Samata anayeichezea Klabu ya Genk amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya katika mchezo ambao Genk wamekubali kipigo cha magoli 6-2 dhidi ya Salzburg.

Samata alifunga goli hilo kwenye dakika ya 52 ya mchezo .Huu ni mwendelezo mzuri wa Samata akiwa na Genk kwani mpaka sasa kafanikiwa kuifungia timu hiyo magoli 6 kwenye msimu huu mpya wa ligi katika mashindano mbalimbali aliyoshiriki.

Mbali na Samata kufunga kwenye mchezo huo Mchezaji Braut Haaland amekuwa kivutio cha wengi baada ya kufanikiwa kufunga magoli 3 kwenye dakika za 2,34 na 45 . Mpaka sasa Haaland kafanikiwa kufunga magoli 16 katika michezo 9 ambayo kashacheza.

Matokeo ya Michezo mingine

Napoli 2- Liverpool

Inter Milan 1-1 Slavia Prague

Borrusia Dortmund 0-0 Barcelona

Lyon 1-1 Zenit Petersburg

Benfica 1-2 RB Leipzig

Ajax 3-0 Lille

Chelsea 0-1 Valencia

Leave a Comment