Safari ya Shiza Kichuya Misri kuleta kina kichuya 6 wengine samba.

Safari ya Shiza Kichuya Misri kuleta kina kichuya 6 wengine samba.

Winga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea club ya Simba SC Shiza Ramadhan Kichuya tayari amekamilisha usajili wa kujiunga na club ya Pharco inayoshiriki Ligi daraja la pili Misri.

Kichuya amejinga na Pharco ya Misri lakini baada ya kukamilisha usajili huo ametolewa kwa mkopo katika club ya Enppi inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri, uhamisho wa Shiza Kichuya umekamilishwa wakati huu mchezaji huyo akiwa kaenda Alexandria Misri kucheza mchezo wake wa CAF Champions League.

Kichuya sasa atapata fursa na kuungana na watanzania wenzake katika Ligi Kuu Misri ambao ni Himid Mao anayecheza Petrojet aliyojiunga nayo akitokea Azam FC na Yahya Zayd aliyejiunga na Ismaily akitokea Azam FC pia, timu ya Kichuya ENNPI kwa sasa ipo nafasi ya 14 ikiwa na point 21.

CEO wa Simba anathibitisha hilo
“Kichuya ameuzwa Pharco lakini anatolewa kwa mkopo Enppi, Matajiri wa Petrol waliopo Premier League! Mshahara wake hata kama angekuwa mwanao ungemruhusu aende tu, Umri wa kucheza mpira sio mrefu hivyo Mtambue tunaofanya maamuzi tuna taarifa zaidi ya hizi mnazozifamu kwa sababu taarifa zingine ni za kimkataba, Na huu ni Mkataba mrefu wa miaka minne! Nimekumegea kidogo tu! Na pia Klabu tutakachovuna si haba tunaweza nunua Kichuya hata 6!. Kwa maana hiyo Shiza Kichuya hatoonekana tena na klabu Simba kwa sasa baada ya kupata mwajiri wake mpya.”

Leave a Comment