Safari ya Mbwana Samatta kuelekea ufungaji bora ubelgiji

Safari ya Mbwana Samatta kuelekea ufungaji bora ubelgiji

MSHAMBULIJAI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa jana ameifungia bao la kwanza klabu yake, KRC Genk katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Waasland-Beveren kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Freethielstadion mjini Beveren.

Samatta alifunga bao lake hilo dakika ya 59, kabla ya Alejandro Pozuelo Melero kufunga la pili dakika ya 82 kufuatia Boljevic kuanza kuwafungia wenyeji dakika ya 11.
Kwa ushindi huo, Genk wanaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi zao 54, ikifuatiwa na Antwerp yenye pointi 45, baada ya zote kucheza mechi 24.

Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana amefikisha jumla ya mabao 57 katika mechi 142 za mashindano yote alizoichezea KRC Genk tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Leave a Comment