Real Madrid yakosa fursa ya kupanda nafasi ya pili La Liga

Real Madrid yakosa fursa ya kupanda nafasi ya pili La Liga

Real Madrid ilikosa fursa ya kupanda hadi nafasi ya pili katika jedwali la ligi ya La Liga baada ya Girona kutoka nyuma na kuwalaza mabingwa hao wa Ulaya uwanjani Bernabeu.

Casemiro alifunga bao la kwanza kupitia krosi iliopigwa na Toni Kroos kutoka wingi ya kulia na kuwapatia wenyeji hao uongozi, Penalti ya Cristhian Stuani ilifanya mambo kuwa 1-1 baada ya Sergio Ramos kushika mpira katika eneo la hatari .

Portu baadaye alifunga bao la ushindi kwa kichwa alichoruka baada ya mkwaju wa Anthony Lozano kupanguliwa na mlinda mlango ,Mambo hayakwenda vizuri kwa ramos baada ya kutolewa nje katika muda wa majeruhi kwa kupewa kadi mbili za manjano.

Beki huyo alikuwa tayari amepewa kadi ya manjano wakati aliposababisha penalti na akapewa onyo wakati alipojaribu kupiga ‘bicycle kick’ lakini akamuumiza mchezaji wa Girona Pedro Alcala.

Real, ambaye alianza wikendi katika nafasi ya pili katika jedwali sasa wako nafasi ya tatu , wakiwa na pointi tisa nyuma ya viongozi Barcelona ambao walishinda 1-0 dhidi ya Real Valladolid siku ya Jumamosi.

Atletico Madrid sasa iko katika nafasi ya pili ikiwa pointi mbili juu ya wapinzani wao Real kufuatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano.

Leave a Comment