Pro Piacenza yalazwa 20-0 katika mechi ya ligi Serie C

Pro Piacenza yalazwa 20-0 katika mechi ya ligi Serie C

Klabu hiyo ya ligi ya Serie C iliowekwa katika kundi A ilishindwa magoli 20-0 na wapinzani wao katika ligi hiyo Cuneo siku ya Jumapili jioni.

Walikuwa nyuma kwa magoli 16 kwa bila wakati wa muda wa mapumziko huku mshambuliaji wa Cuneo Hicham Kanis akifunga magoli sita pekee kabla ya mapumziko naye mshambuliaji mwenza Eduardo Defendi akipata magili matano.

Katika safu ya ulinzi ya Pro Piacenza kulikuwa na matatizo yaliosababisha mvua hiyo ya magoli. Wakiwa chini katika ligi hiyo ya tatu ya Itali, klabu hiyo ya kaskazini ina matatizo makubwa ya ufadhili.

Walipokonywa pointi nane mapema katika kampeni yao na wameripotiwa kushindwa kuwalipa wachezaji wao tangu mwezi Agosti hatua iliosababisha kujiuzulu kwa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza.

Walishindwa kushiriki katika mechi tatu kabla ya kichapo hicho cha siku ya Jumapili na iwapo hawangeshiriki ingesababisha kupigwa marufuku katika ligi hiyo ya Serie C.

Pro Piacenza walilazimika kuanza mechi hiyo wakiwa na wachezaji saba pekee wakiwempo vijana sita. Huku wakikosa mkufunzi, nahodha wao mwenye umri wa miaka 18 Nicola Cirigliano alilazimika kuchukua wadhfa wa ukufunzi.

Walimaliza mechi hiyo wakiwa na mchezaji mwengijne wa ziada baada ya mmoja ya wachezaji hao kufanikiwa kupata nyaraka za utambulisho wake baada ya mechi kuanza.

Gabriele Gravina, rais wa shirikisho la soka nchini Itali alitaja matokeo ya siku ya Jumapili kama ‘matusi kwa soka’, ‘‘Katika kisa kama hiki Shirikisho la soka nchini Itali ilikuwa na jukumu la kutilia mkazo sheria zote’‘, alisema. ‘‘Jukumu letu ni kulinda hamu ya mashabiki , afya, biashara na uaminifu wa ligi hii. Tulichoshuhudia itakuwa aibu ya mwisho’‘.

Leave a Comment