Paul Scholes ameanza vizuri kazi yake ya ukocha

Paul Scholes ameanza vizuri kazi yake ya ukocha

Paul Scholes ameanza vizuri kazi yake ya ukocha baada ya kikosi chake cha Oldham kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Yeovil.

Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya Scholes, akiwa kocha katika benchi baada ya kuingia rasmi katika kazi hiyo.

Scholes ni kiungo nyota wa zamani wa Manchester United, Pia alikuwa staa wa Man United aliyefanya vizuri katika club toka alipokuwa kwenye Academy ya Man United kuanzia mwaka 1991 hadi 1993, baada ya hapo akaanza kuingia kwenye kikosi cha wakubwa cha Man United alichodumu nacho hadi mwaka 2013 alipoamua kustaafu.

Leave a Comment