Oussama Idrissi afanya maamuzi magumui, sasa kuvaa jezi ya Morroco

Oussama Idrissi afanya maamuzi magumui, sasa kuvaa jezi ya Morroco

Winga wa AZ Alkmaar Oussama Idrissi amefanya maamuzi magumu kwa kuweka pembeni fursa ya kuichezea team ya taifa ya Uholanzi na badala yake ataitumikia taifa la Morocco na si Uholanzi

Oussama Idrissi mwenye umri wa miaka 22 alikubali mwaliko wa kujiunga na kambi Morocco mwezi Novemba 2018 lakini hakufanya uchaguzi wa mwisho.

Oussama Idrissi ameitumikia Uholanzi U21 kwa muda na hakupata bahati ya kutumikia kikosi cha Uholanzi kamili, sasa atakuwa huru kutumikia jezi ya Morocco na anaweza kuchaguliwa kwenye mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Malawi mwezi Machi.

Idrissi imefunga mabao 13 na kusaidia 17(assists) katika michezo 28 ya AZ Alkmaar msimu huu

Leave a Comment