Neno la Mo mbele ya waandishi wa habari

Neno la Mo mbele ya waandishi wa habari

Mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji leo amekutana na waandishi wa habari kuzungumza mambo mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo ikiwa ni pamoja na mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Simba na Al Ahly siku ya Jumanne February 12, 2019.

Mo ameeleza pia kuhusu mpango walionao wa kuimarisha benchi lao la ufundi kwa ajili ya kuleta ushindani.

“Sisi kama Bodi ya Wakurugenzi wa Simba tulijipangia mipango ya muda mfupi, kati na muda mrefu.”

“Kama mnakumbika Simba katika miaka mitano iliyopita tulikuwa hatujapata ubingwa lakini mwaka jana tulifanikiwa, hiyo ilikuwa plan yetu ya muda mfupi.”

“Mwaka huu kipaumbele chetu ni kutetea ubingwa wetu ili tuweze kushiriki Champions League ya mwaka ujao. Hiyo ilikuwa plan ya muda mfupi.”

“Tumepanga kiingilio cha shilingi 2000 kwa majukwaa ya mzunguko ambapo mechi ya mwanzo kiingilio kilikuwa ni shilingi 5000.”

“Kesho asubuhi tutatangaza rasmi viingilio vyote vya mechi yetu na Al Ahly siku ya Jumanne.”

“Mwaka huu shabaha yetu mwanzoni ilikuwa ni kufika hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika lakini tumefika hapa na tumekuja kushindana.”

“Kwenye mpira kuna mambo ambayo yanatokea hayapo kwenye plan, sote tunafahamu Shomari Kapombe ameumia, Erasto Nyoni ameumia, kwa namna moja au nyingine imetutingisha.”

“Tunashindana na klabu ambazo zina budget kubwa, zina uzoefu mkubwa kwenye mashindano ya Afrika.”

“Ukiongelea Al Alhy unaweza kuifananisha na Real Madrid kwenye mataji. Juzi nimesikia kwamba Al Ahly wamemnunua mchezaji kwa kwa zaidi ya Tsh. bilioni 10 na alitoa pasi tatu za mwisho kwenye mechi tuliyochezanao.”

“Kwa hiyo tunashindana na klabu kubwa, hiyo AS Vita tukiiongelea mwaka jana walifika fainali.”

“Tutatangaza afasi za kazi lakini kwa kifupi tutaimarisha zaidi benchi zima la ufundi kwa kuzidisha uwezo. Mo Dewji akijibu swali aliloulizwa kuhusu Simba kutokuwa na kocha msaizi.”

Leave a Comment