Mwili wa Emiliano Sala watambuliwa

Mwili wa Emiliano Sala watambuliwa

Mwili ulioopolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoanguka ni wa mchezaji soka wa timu ya Cardiff City, Emiliano Sala Polisi ya Dorset imethibitisha.

Sala, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akisafiri kwenda Cardiff ikatika ndege ambayo rubani wake alikuwa ni David Ibbotson, iliyopotea mnamo Januri 12.

Mwili wake ulipatikana Jumatano baada ya kugunduliwa kwa mabaki ya ndege hiyo Jumapili asubuhi.

Katika taarifa yake, kikosi hicho kimesema: “mwili ulioletwa katika bandari ya leo Alhamisi Februari 7 2019, umetambuliwa rasmi kuwa wa mchezaji soka Emiliano Sala.

“Familia ya Sala na rubani David Ibbotson wamearifiwa kuhusu taarifa hii na wataendelea kupewa usaidizi na maafisa wa kitengo maalum.”

Hata hivyo, mabaki ya ndege hiyo yalipatikana chini ya bahari baada ya wasamaria wema kuchangisha fedha zilizowezesha operesheni ya binafsi iliyoongozwa na mwanasayansi ya bahari David Mearns.

Juhudi za kuinyanyua ndege hiyo toka chini ya bahari zimeshindikana kwa sasa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Leave a Comment