Mshahara wa pauni elfu 400 kwa wiki wampeleka Aaron Ramsey Juventus

Mshahara wa pauni elfu 400 kwa wiki wampeleka Aaron Ramsey Juventus

Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Juventus msimu ujao kwa katika cha pauni £400,000 kwa wiki.

Nyota huyo wa miaka 28 amekubali mkataba wa miaka minne utakaomwezesha kujiunga na ligi ya champions ya Italia bila malipo baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 11.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales unakamilika Juni 30 na Gunners hawatapokea malipo yoyote atakapo ondoka.

Arsenal imesema mchango wa Ramsey ulikuwa mkubwa sana katika klabu hiyo na kuongeza kuwa “atakasalia katika kumbu kumbu ya historia” ya mashabiki.

Akiandika katika mtandao wake Instagram, Ramsey aliwashukuru mashabiki wa Arsenal na kusema kuwa"ataendelea kuwaunga mkono 100%”.

“Mlinikaribisha katika klabu hiyo nikiwa kijana mdogo na nimeshuhudia nyakati nzuri na mbaya.

“Nasikitika kuondoka baada ya miaka 11 ya ufanisi sijui nielezee vipi hisia zangu muda huu. Asanteni.

Tuvuti ya Juventus imemkaribisha Ramsey kwa kuandika kwamba atakuwa mkazi wa Wales wa tatu kuiwakilisha klabu hiyo baada ya John Charles na Ian Rush.

Leave a Comment