breaking news New
Mourinho ahukumiwa mwaka mmoja jela

Mourinho ahukumiwa mwaka mmoja jela

Kocha wa zamani wa Mancester United Jose Mourinho amekubali adhabu ya kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la ukwepaji kodi nchini Uhispania.

Kwa nchi ya Uhispania huwa haiwafungi jela wahalifu ambao wamehukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili na wale ambao hawajatumia mabavu kwenye kutenda uhalifu wao.

Mourinho ambaye amekiri makosa yake, anatarajiwa kulipa faini ya Euro 182,500 (£160,160) ili kujihakikishia kuwa hatupwi jela.

Kwa ujumla Mourinho ametozwa faini ya Euro milioni 2 kama adhabu ya kukwepa kodi.

Wendesha mashtaka walimtuhumu kocha huyo kukwepa kodi ya Euro milioni 3.3m (£2.9m) katika kipindi ambacho alikinoa kikosi cha Real Madrid Real Madrid kati ya 2011-2012.

Mourinho anatuhumiwa kuanzisha makampuni kadhaa visiwani British Virgin Islands ili kusimamia mapato yake yatokanayo na picha.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa makampuni hayo yaliundwa ili kuficha mapato halisi ya mkufunzi huyo na kuathiri kiasi cha kodi alichotakiwa kulipa.

Makubaliano ya adhabu hiyo yalifikiwa na Mourinho na maafisa kodi hapo awali, na leo walienda mahakamani ili kuyapa uhalali wa kisheria.

Kocha huyo ni nyota mpya wa mchezo wa soka kufikia makubaliano na watoza kodi wa Uhispania kwa tuhuma za ukwepaji wa kodi.

Mwezi Januari Cristiano Ronaldo alikubali kulipa faini ya Euro milioni 18 kuepuka kifungo cha miezi 23, katika kesi ya mapato ya picha pia.

Ronaldo alitenda makosa hayo mwaka 201 mpaka 2014 kipindi ambacho Mourinho alikuwa akikinoa kikosi hicho.

Leave a Comment