Miguel Almiron avunja rekodi ya uhamisho Newcastle

Miguel Almiron avunja rekodi ya uhamisho Newcastle

Newcastle imevunja rekodi yake ya miaka 14 ya uhamisho kwa kumsajili mchezaji raia wa Paraguay Miguel Almiron kutoka Atlanta United.

Almiron mpaka anaicha Atlanta United amefunga magoli 22 katika mechi 62 alizocheza kwenye club hiyo , Awali alihusishwa na tetesi za kuchukua mikoba ya Ramsey pale Arsenal huku west ham wakijaribu bahati yao bila mafanikio.

Almiron ni aina ya mchezaji mwenye kupenda soka la kushambulia kwa kasi huku akitumika vizuri sana kwenye eneo la tatu ya juu ya kiwanja ukichagizwa na uwezo wake wa kupiga mpira umbali wotewote kwa ubora ule ule , kwa mujibu wa takwimu huwa anafika viwango wastani wa 7.82 akiwa kwenye eneo la juu ya uwanja.

Almiron aliwahi pia kuwa bingwa wa ligi ya Argentina mnamo 2016 baada ya kuicheza Lanus mechi 12 katika divisheni ya Primera.

Uhamisho wa Miguel Almiron kuingia Newcastle unamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kuuzwa kutoka ligi kuu ya soka Marekani.

Tulikuwa tunamfukuzia Miguel Almiron kwa muda, amesema meneja wa Newcastle Rafael Benitez. Tuliona mchezaji aliye na kasi katika ushambuliaji, anayeweza kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Leave a Comment