Michuano ya vijana wasiozidi miaka 20 Africa yaendelea

Michuano ya vijana wasiozidi miaka 20 Africa yaendelea

Timu ya taifa ya Afrika Kusini yenye vijana wasiozidi miaka 20, wanaingia uwanjani kumenyana na Nigeria katika mchuano wa pili, kuwania taji la bara Afrika.

Mashindano haya yaliyoanza mwishoni mwa wiki iliyopita, yanafanyika nchini Niger.

Afrika Kusini wanacheza mechi yake ya pili baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na wenyeji Niger.

Nigeria nao walianza vema baada ya kuwashinda Burundi, mabao 2-0.

Mechi nyingine itakayochezwa baadaye siku ya Jumanne, vijana wa Burundi watamenyana na wenyeji kutafuta ushindi wa kwanza.

Kesho, itakuwa ni zamu ya kundi B, Mali itachuana na Burkina Faso huku Ghana ikicheza na Senegal.

Leave a Comment