Mbwana Samatta kifua mbele mechi ya hisani “Samakiba”

Mbwana Samatta kifua mbele mechi ya hisani “Samakiba”

NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Ally Samatta na Rafiki zake wameibuka na ushindi wa mabao 6-3 dhidi ya Mwanamuziki nyota nchini, Allly Saleh Kiba na Rafiki zake katika mechi ya Hisani jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Mabao ya Team Samatta lepo yamefungwa na Samatta mwenyewe mawili dakika za 15 na 40, beki wa Nkana FC ya Zambia, Hassan Kessy kwa penalti dakika ya tano, mshambuliaji JS Saoura ya Algeria, Thomas Ulimwengu dakika ya 38, beki wa Yanga SC, mshambuliaji wa chipukizi Kelvin John ‘Mbappe’ dakika ya 59 na Mpoki dakika ya 79.

Mabao ya Team Kiba leo yamefungwa na winga wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco mawili dakika za 18 na 68 na mshambuliaji Mnyarwanda wa Simba SC, Meddie Kagere dakika ya 21, wakati Abdul Kiba alikosa penalty mfululizo, zote zikichezwa na kipa wa zamani wa Simba, Kabal Faraji.

Hii ni mara ya pili wawili hao, Samatta mchezaji wa KRC Genk ya Ubelgiji na Kiba ambaye pia ni mchezaji wa Coastal Union ya Ligi Kuu ya Bara kufanya tamasha hilo lijulikanalo kama Nifuate baada ya Juni mwaka jana pia.

Lengo ni kukusanya fedha za kwenda kusaidia madawati katika shule za msingi hapa Dar es Salaam.

Leave a Comment