Matokeo : Kagera yapokea kipigo kaitaba, Ruvu Shooting yaondoka na ushindi wa jioni

Matokeo : Kagera yapokea kipigo kaitaba, Ruvu Shooting yaondoka na ushindi wa jioni

TIMU ya Tanzania Prisons imepata ushindi wa ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Ushindi huo ulitokana na mabao ya Jumanne Elfadhili kwa penalti dakika ya 40 na Salum Kimenya dakika ya 90 , Matokeo haya yanafanya Tanzania Prisons ifikishe pointi 20 baada ya kucheza mechi 23, ikijiinua kutoka mkiani kabisa mwa ligi hadi nafasi ya 18. mwanga umeanza kumulika kwenye team chini ya kocha mpya, Mohammed Rishard ‘Adolph’ baada ya kuuanza msimu vibaya chini ya kocha Mohammed Abdallah ‘Bares’ aliyefukuzwa licha ya kushinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita.

Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Mecky Mexime yenyewe inabaki na pointi zake 28 katika mechi ya 22 ikishika nafasi ya 10.

Mechi nyingine za Ligi Kuu ,

Bao pekee la Baraka Mtui dakika ya 85 limeipa ushindi wa 1-0 Ruvu Shooting dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni nje ya kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, mabao ya Ahmed Shiboli dakika ya 33, Hassan Matelema dakika ya 47 na Ally Bilaly dakika ya 90.

Stand United imelazimishwa sare ya 0-0 na timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Leave a Comment