Marouane Fellaini: Nyota wa Manchester United kujiunga na klabu ya China

Marouane Fellaini: Nyota wa Manchester United kujiunga na klabu ya China

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini ameridhia makubaliano binafsi mkataba wa kibinasi na klabu ya Shandong Luneng kwa lengo la kuhamia klabu hiyo ya China.

United wamekataa kutoa tamko lolote ikiwa malipo yoyote yamefikiwa kumnunua mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye alitia saini nao mwaka 2018.

Fellaini, 31, alikuwa mchezaji mkubwa wa kwanza aliyesainiwa baada ya enzi ya Sir Alex Ferguson, akijiunga na Manchester Utd kwa kima cha pauni milioni 27.5 mwaka 2013 akitokea Everton.

Kwa taarifa za awali na tetesi malipo ya fellaini yataongezeka hadi £ 365,000 kwa wiki, maana yake atapata £ 9m kwa mwaka baada ya kodi.

Mwisho wa dirisha la uhamisho wa wachezaji katika ligi ya China ni Februari 28.

Fellaini alitia saini kandarasi mpya ya miaka miwili Old Trafford mwezi Juni mwaka jana lakini hajawahi kukubalika na mashabiki wa United licha ya kukonga nyo za mameneja David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho.

Leave a Comment