Manchester City yarejea kileleni Ligi Kuu England

Manchester City yarejea kileleni Ligi Kuu England

Pep Guardiola anasema kuwa Manchester City wamegundua kutosalimu amri baada ya kurudi katika kilele cha jedwali la ligi kwa mara ya kwanza tangu tarehe 16 Disemba kufuatia ushindi dhidi ya Everton.

Wiki moja iliopita City ilikuwa pointi tano nyuma ya Liverpool lakini ikachukua fursa hiyo baada ya klabu hiyo chini ya ukufunzi wa Jurgen Klopp kupata sare kadhaa na hivyobasi kupanda juu ya miamba hiyo ya Anfield kupitia wingi wa magoli huku wakiwa wamecheza mechi moja zaidi.

Aymeric Laporte alikutana na mkwaju wa adhabu wa David Silva na kucheka na wavu kwa kutumia kichwa hatua ilioiweka mbele City kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika huku bao la pili likifungwa na mshambuliaji Gabriel Jesus dakika ya 90 ya mchezo.

Kwa sasa macho yote yataelekezewa Liverpool ambao wanaweza kupanda katika kilele cha ligi iwapo watapata ushindi dhidi ya Bournemouth siku ya Jumamosi, saa 24 kabla ya City kucheza dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Etihad.

Leave a Comment