Mambo Tuliyojifunza Katika Fainali Ya UCL

Mambo Tuliyojifunza Katika Fainali Ya UCL

Machache niliyoyaona katika fainali ya UCL

Liverpool V Tottenham Hotspurs


1.Allison Becker katika kiwango bora.

Hakuna shaka katika kipindi cha kwanza Tottenham Hotspurs hawakuwa bora katika kushambulia kwani hawakufanikiwa kupiga shuti lolote ambalo lilifanikiwa kuweza kulenga lango la Liverpool.

Kipindi cha pili Tottenham Hotspurs walilejea na kushambulia kwa kasi sana huku Allison akiweza kuokoa michomo hatari katika lango lake ambayo kuna uwezekano mkubwa kama Spurs wangefunga goli taswira ya mchezo ingebadilika.

Ubora wa Allison ulikuwa katika mambo yafuatayo Awareness ,Concentration na fantastic co-ordination, Uwezo wa kupunch mipira pamoja na Wepesi wake.

Kwangu Mimi huyu ndiye mchezaji bora wa mchezo wa fainali.

2.Harry Kane hakuwa katika kiwango kizuri.

Kukaa nje ya Uwanja kwa wiki kadhaaa huku akiwa anasumbuliwa na majeraha ni moja kati ya kitu ambacho kimeathiri kiwango cha Harry Kane katika mchezo wa fainali kwani alikuwa katika kiwango cha kawaida kutokana na kukosa Game Fitness.

3.Robertson katika kuipa timu uwiano sawa ndani ya Uwanja.

Achana na uwezo wake mkubwa wa kupiga Krosi akiwa ndani ya uwanja katika mchezo wa fainali alikuwa na umuhimu mkubwa kwani aliipa uwiano ulio sawa klabu ya Liverpool kuanzia katika kujilinda lakini hata pale Liverpool walipokuwa wanashambulia alionekana kutimiza vyema majukumu yake.

Tofauti yake na Trent Anord usiku wa fainali ilikuwa ni ngumu kwa Anord kuweza kushambulia kutokana na katika nafasi yake alikuwa anacheza dhidi ya Danny Rose pamoja Na Son ambaye alionekana kuzunguka eneo kubwa la Uwanja.

4.Kloop anazidi kufanikiwa na matumizi ya Origi kama mchezaji wa akiba.

Matumizi ya Origi akianza kama mchezaji wa akiba katika kikosi cha Liverpool yamekuwa na faida kubwa kwa klabu hiyo kutokana na kuwa na mchango mkubwa sana katika kubadili Matokeo kwenye kipindi ambacho klabu inakuwa inamhitaji.

Rejea mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Barcelona ambao Liverpool walishinda 4-0 kisha katika mchezo wa Jana dhidi ya Tottenham ni mwendelezo wa kiwango kizuri cha Origi akianza kama mchezaji wa akiba.

Hakuna shaka Kloop kafanikiwa msimu huu katika hili tofauti na msimu uliopita ambapo timu ilionekana kukosa mbadala wa wachezaji katika maeneo mengi.

5.Kloop avunja gundu katika mashindano ya Ulaya.

Kloop kapoteza fainali kadhaa za Ulaya akiwa na Liverpool kapotea fainali ( dhidi ya Bayern Munich ,Seville na Real Madrid ). Kutwaa taji hili kwa msimu huu ni tafsiri kuwa Kocha Huyo kafanikiwa kuondoa gundu.

6.Liverpool wanaweza kubeba Treble msimu huu?

Baada ya kukosa kutwaa taji la ligi kuu ya Uingereza na kufanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya kunawapa nafasi ya Liverpool kufuzu kucheza katika fainali 2 kubwa ,Moja ni dhidi ya Chelsea katika kombe la UEFA Super Cup lakini Kombe lingine ni klabu bingwa ya Dunia.Je Liverpool watafanikiwa?

©Timotheo S John | Mwanza
Simu namba 0763972038

Leave a Comment