breaking news New
Mambo 10 unayopaswa kuyafahamu kuelekea michuano ya Copa America

Mambo 10 unayopaswa kuyafahamu kuelekea michuano ya Copa America

Michuano ya Copa Amerika inatarajia kuanzia tarehe 14 mwezi huu mpaka tarehe 7 mwezi July ,Michuano hiyo hushirikisha timu kutoka katika nchi za Amerika ya Kusini. Yafuatayo ni mambo unayoapaswa kuyafahamu Kuelekea katika mashindano hayo.

1.Copa America ndio Michuano mikongwe zaidi duniaani kwa ngazi ya Timu za taifa kwani Michuano hii ilianzishwa mwaka 1916 mpaka sasa ikiwa inatimiza jumla ya miaka 103.

2.Timu ya taifa ya Uruguay ndio timu ambayo imefanikiwa kutwaa taji hilo Mara nyingi zaidi ikiwa imefanikiwa kutwaa Mara 15.

3.Katika mashindano ya mwaka huu yatashirikisha jumla ya timu 12 ( Timu 10 kutoka Amerika ya Kusini na timu 2 zikiwa zimealikwa ambazo ni Japan na Qatar ).Ushiriki wa Japan na Qatar katika mashindano hayo imetokana na kuwa timu za Uhispania na Ureno ambazo zilitakiwa zialikwe katika mashindano haya zinashiriki mashindano kama ligi ya mataifa barani Ulaya na kufuzu fainali za Uero kwa mwaka 2020.

4.Chile ndiye bingwa mtetezi katika kombe hilo akiwa kafanikiwa kutwaa taji hilo Katika miaka 2 mfululizo yaani mwaka 2015 na 2016 na katika
fainali zote amefanikiwa kushinda dhidi ya Argentina.

5.Timu shiriki katika mashindano ya mwaka huu ni Argentina ,Bolivia ,Brazil ,Chile ,Colombia ,Ecuador ,Paraguay ,Peru ,Uruguay ,Venezuela
,Qatar na Japan.

6.Mashindano yatakuwa na jumla ya waamuzi 46 huku mataifa 10 ambayo ni timu wenyeji kila taifa limetoa waamuzi ,Lengo likiwa ni kwa ajili ya
kukuza viwango vya waamuzi katika kila nchi na kuhamasisha uhusiano mwema kati ya nchi moja dhidi ya nyingine.

7.Brazil ndiye nchi mwenyeji aliyeandaa mashindano haya na yatafanyika katika miji 5 tofauti ambayo ni Salvador ,Belo Horizonte ,Sao
Paulo ,Rio Da Janeiro ,Porto Alegre.Uwanja unaobeba watazamaji wengi zaidi ni uwanja wa Maracana unaobeba watazamaji 74,738 uliopo katika mji wa Rio De Janeiro na uwanja mdogo ni Itaipava ambao unauwezo wa kubaba watazamaji 51,900 pekee.

8.Mashindano ya mwaka huu ni mashindano ya mwisho kufanyika katika mwaka ambao haugawanyiki kwa 2 ,Kuanzia mwaka 2020 mashindano haya ya Copa America yatakuwa yakifanyika mwaka sawa na ambao mashindano ya Ligi ya UERO ( UEFA European Championship ) pia katika mashindano ya mwaka 2016 yalitokea kwa muda mmoja kwa kuwa CONMEBOL waliamua kufanyika kwa mashindano hayo kwa ajili ya kuadhimisha sherehe ya kutimiza miaka 100 ya mashindano hayo.

9.Endapo Chile watafanikiwa kutwaa taji hilo kwa mwaka huu basi watafikia rekodi ya Argentina ya kutwaa taji hilo Mara 3 mfululizo walipofanikiwa kufanya hivyo kati ya mwaka 1945,1946 na mwaka 1947.

10.Eduardo Vargas ambaye anaichezea timu ya taifa ya Chile ndiye mshambuliaji pekee katika mashindano haya ambaye anashiriki mpaka sasa
anaeshirikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja ( Magoli 5 )

Leave a Comment