breaking news New
Makipa bora kuwahi kutokea Duniani

Makipa bora kuwahi kutokea Duniani

Karibu katika mwanzo wa masimulizi ya wachezaji waliofanya vizuri katika historia ya mpira wa miguu kwa nyakati tofauti . Leo tunatazama makipa 5 bora waliofanya vizuri katika mpira wa miguu kwa nyakati tofauti.Wafuatao wanatajwa kuwa kama makipa bora duniani kwa wakati wote na orodha yao ni kama ifuatavyo

5.Dinno Zoff (ITALIA)

Zoff ni mchezaji mkongwe zaidi kushinda taji la kombe la dunia , alifanya hivyo akiwa na miaka 40 wakati huo akiwa nahodha wa timu ya taifa ya Italia. Ikumbukwe kuwa alicheza dakika 1142 bila kuruhusu goli kwenye michezo ya kimataifa , rekodi ambayo haijavunjwa mpaka leo.

Michezo 112 kwa timu ya taifa , mafanikio kwenye taji la EURO mwaka 1968 , Kombe la dunia mwaka 1982 huku akishinda taji la Serie A mara 6 ,Makombe 2 ya Italia na taji moja la Ulaya.

Zoff anatajwa kama kipa namba 3 kwa ubora kwenye karne ya 20 katika kura zilizopigwa na wadau wa soka kwenye mtandao wa IFFHS na mwaka 2003 alitajwa kama mchezaji bora wa kitaliano katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

4.Sepp Maier (UJERUMANI)

Moja kati ya wachezaji bora kwa kizazi chao akiungana na Franz Beckenbauer kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani na kwenye klabu ya Bayern Munich. Alishinda mataji ya ligi kuu ya ujerumani na kombe la ujerumani mara 4 huku akishinda mataji ya Ulaya mara 3 mfululizo , Huku kwa ngazi ya timu ya Taifa akifanikiwa kutwaa taji la Ulaya mwaka 1972 na kombe la dunia mwaka 1974.

Lakini kwa tuzo binafsi alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Ujerumani ya Magharibi mara 3. Mafanikio yake makubwa yalitokana na mwendelezo wa ubora wake na kuwa na afya njema .Kati ya Mwaka 1966 mpaka 1977 alifanikiwa kucheza michezo 422 mfululizo bila kukosa mchezo wowote kwa miaka 11.

3.Gordon Banks ( ENGLAND)

Banks anakumbukwa zaidi kwa kufanikiwa kuokoa mchomo wa Pele mwaka 1970 kwenye kombe la Dunia .Ingawa katika kizazi chake hakufanikiwa sana katika utwaaji wa mataji , Ubora wake ndio unamfanya kutambulika kama miongoni mwa nakipa bora kwa kizazi chao.

Banks anashikilia rekodi ya kuwa kipa pekee toka England kufanikiwa kutwaa taji la kombe la Dunia .Maisha yake ya soka yalianza kwenda kombo baada ya kupata ajali ya gari hali iliyopelekea kuwa na tatizo kwenye macho huku uwezo wa kuona ukipungua , Alijaribu kupambana ili kurejea kwenye ubora wake lakini ilishindikana.

Alimaliza maisha yake ya soka akiwa kacheza michezio 73 pekee kwa timu ya Taifa huku akitajwa kuwa kama kipa namba 2 kwa ubora kwa karne ya 20 katika kura zilizopigwa kwenye mtandao wa IFFHS.

2.Peter Schmeichel (DENMARK)

Mafanikio makubwa ya klabu ya Manchester United katika miaka ya 1990 yalitokana na kipa huyu , lakini ikumbukwe kuwa hata kabla ya mafanikio hayo tayari alikuwa kafanikiwa na klabu ya Broendby IF akishinda mataji 4 ya Denmark.

Alianza kujulikana Ulimwenguni mwaka 1992 akiisaidia timu ya Denmark kuibuka mabingwa wa Taji la Ulaya , Lakini akiwa Manchester United alishinda mataji 5 ya ligi kuu , Mataji 3 ya FA ,Kombe la ligi na taji la Ulaya mara 1.

Mchezo wake wa mwisho ilikuwa mwaka 1999 alipofanikiwa kutwaa treble akiwa na manchester United. Ikumbukwe kuwa alitajwa kuwa kipa bora ulimwenguni mara 2 na mtandao wa IFFHS.

1.Lev Yashin (URUSI)

Aliitwa Spider Man katika kizazi chake kwa kuwa alionekana ni kama kuwa na mikono 8 kwa ajili ya kuokoa michomo .Hakuna kipa kama yeye kuwahi kutokea katika dunia ya soka.

kwanza huyu jamaa alichezea klabu moja pekee ambayo ni Dynamo Moscow , huku akiitumikia timu ya USSR michezo 74 pekee. Yashin aliokoa penati zaidi ya 150 huku akiwa na Clean Sheets zaidi ya 500 huku akicheza michezo 812 pekee.

Alifanikiwa kushinda tuzo ya kipa bora wa USSR mara 3 , huku akisalia kuwa kipa pekee aliefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya , akifanya hivyo mnano mwaka 1963.

mwaka 200 alitajwa kuwa kama kipa bora zaidi wa karne ya 20 katika kula zllizopingwa kwenye mtandao wa IFFHS

Leave a Comment