breaking news New
Mabadiliko Makubwa VPL 2019/2020

Mabadiliko Makubwa VPL 2019/2020

Ligi kuu ya Tanzania Bara imeishaanza kutimua vumbi kwenye viwanja tofauti tofauti kwa nchi nzima . Tofauti ya ligi ya msimu uliopita na msimu huu upo kwenye maeneo kadhaa kuanzia kanuni ambazo zinawaongoza waalimu na mabenchi mbalimbali ya ufundi ,Udhamini katika ligi pamoja na Mabadiliko kwa timu ambazo zinatarajia kushuka daraja.

Maakala hii tunatazama kwa namna baadhi ya mabadiliko kwenye ligi kuu ya mwaka huu yatakavyopelekea ligi kuwa na ushindani tofauti na msimu uliopita wa 2018/2019

1.Idadi ya timu zitakazoshuka daraja

Msimu huu kanuni zimebadilika na kupelekea kuwa na mabadiliko kwa timu ambazo zitashuka daraja . Msimu huu timu 4 zitashuka daraja moja kwa moja yaani toka timu ya 17 mpaka ya 20 kwenye msimamo wa ligi kuu na timu ambazo zitashika nafasi ya 15 na 16 zitacheza mchujo dhidi ya timu kutoka ligi daraja la Kwanza.

Mabadiliko hayo yanatarajia kufanya ligi kuwa na ushindani tangu mwanzo mwa ligi mpaka mwisho wa ligi ili timu kukwepa lushuka daraja . Ukitazama msimu uliopita ligi ilikosa mvuto kutokana na idadi kubwa ya timu kupambania kushuka daraja katika dakika za mwisho kuliko kupambania Ubingwa wa ligi kuu.

2.Nafasi za kuwakilisha Taifa kimataifa.

Kwa sasa taifa la Tanzania linawakilishwa na timu nne kimataifa timu 2 kwenye ligi ya mabingwa Barani Afrika na timu 2 kwenye kombe la mataifa Shirikisho .Mfumo wa awali ulifanya nafasi ya kwanza kwenye ligi kugombewa zaidi l;akini kwa sasa kuanzia nafasi ya kwanza mpaka ya tatu hupambaniwa na timu ili kupata nafasi ya kushiriki kimataifa.

Lakini pia kwenye kombe la Azam Sports Federarion tunatarajia kuwepo kwa ushindani mkubwa kwa ajili ya kuwakilisha taifa kwenye kombe la shirikisho Barani Afrika.

3.Kurejea kwa Udhamini ligi kuu.

Ligi kuu kwa msimu uliopita ilikuwa na wadhamini wengine ambao waliweza kudhamini ligi na vilabu kwa ujumla kama KCB Bank pamoja na Azam Media Limited lakini kurejea kwa udhamini mkuu kutafanya vilabu kuwa na uhakika wa mapato ambayo yatawasaidia katika shughuli mbalimbali za uendeshwaji wa klabu kwa msimu huu.

Lakini pia uwepo wa wadhamini binafsi katika timu husika ni chachu kwa klabu kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato ukiachana na kutarajia viingilio vya mashabiki ndani.

Leave a Comment