breaking news New
Liverpool yaendelea kudondosha point

Liverpool yaendelea kudondosha point

Sare mbili mfululizo ambazo Liverpool wamezipata katika mechi zao za Ligi ya Premia hivi karibuni zinazidi kufanya mpambano wa kunyakuwa ubingwa kuwa mgumu zaidi.

Hali hiyo inaanza kukumbushia machungu ya mashabiki wa Liverpool kwa misimu ya 2008-09 na 2013-14 ambapo timu yao ilipokwa tonge mdomoni katika dakika za mwisho.

Liverpool, maarufu kama majogoo wa jiji hawajanyanyua ubingwa wa Ligi ya England toka mwaka 1990.

Mara mbili katika wiki nne zilizopita Liverpool ilikuwa na nafasi ya kutanua pengo la uongozi kileleni mwa Ligi ya Premia kwa alama kubwa hali ambayo ingewafanya wawe na nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa.

Liverpool walikuwa na wasaa wa kutanua pengo kwa alama 7 laiti wangeliwafunga Leicester City siku moja mbele. Hata hivyo Liverpool ilitoka sare ya 1-1 katika mchezo huo uliopigwa Januari 30, na kufanya pengo liwe alama tano.

Klopp alilama kuwa theluji iliyokuwa imedondoka uwanjani iliwazuia kupata matokeo bora uwanjani.

Jana Liverpool ilirejea tena dimbani dhidi ya West Ham ambapo walitoka sare ya 1-1 tena. Wikendi, City waliwabamiza Arsenal goli 3-1, hivyo kwa matokeo hayo pengo sasa limepunguwa mpaka alama tatu baina yao.

Hili ni anguko kubwa kwa Liverpool na habari njema kwa Man City. Tofauti kati yao ilikuwa alama tisa Disemba 29. Endapo Man City itashinda mchezo wake dhidi ya Everton kesho Jumatano wataongoza msimamo wa Ligi ya Premia kwa tofauti ya magoli. Tottenham pia bado wangali katika mbio za kusaka ubingwa wakiwa na alama 57, alama tano tu nyuma ya Liverpool.

Swali je liverpool wanaweza kwendana na kasi ya ligi kwa match 13 zilizo baki bila kudondosha point ?

Leave a Comment