breaking news New
Liverpool na Senegal zinamdai Sadio Mane

Liverpool na Senegal zinamdai Sadio Mane

Inachukua muda kupata kile unakihitaji kwa nia zote, hii ni pamoja na kuunganisha sala na juhudi juu ya kile unachokitafuta, Hii inajidhirilisha kwa ustadhi Sadio mane. Kwa sasa ni mshambuliaji wa klabu ya liverpool akiambatana na nyota wa Misri Mohamad Salah pamoja Roberto Firmino raia brazil. Muunganiko wao umekuwa hatari sana kipindi cha hivi karibuni. Kongole kwa mjeruman jurgen kloop ambaye ni mwalimu wa klabu hapo hebu turudi kumuangazia nyota wetu wa leo.

Alizaliwa tarehe 10 april 1992,Wengi watajiuliza kafikaje klabuni Liverpool. Hii safari sio ya kitoto, ilianzia Nchini ufaransa katika Akademi ya Metz hapo ndipo chimbuko la nyota huyu lilipo anzia. Mnamo mwaka 2012, jicho la klabu ya Redbull Salzburg ya nchini Austria ikamuona kinda huyo. Akaitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili. Wakashinda Bundesliga ya Austria na Austria Cup mwaka 2014.

Hapo ndipo akakutana na mshambuliaji wa Italy Pelle. Klabuni hapo sadio mambo yalimnyookea na kuonyesha kiwango kikubwa kilicho sisimua mashabiki wa klabu hiyo. Alijiwekea rekodi ya Ligi Kuu kwa kasi ya kufunga kofia(hat-trick) wakati alifunga mara tatu katika sekunde 176 wakati wa kushinda 6-1 dhidi ya Aston VillaNdipo msimu wa ligi ya uingereza mwaka 2016/17 kipindi cha usajili dirisha kubwa sadio alimwaga wino katika karatasi za majogoo wa jiji kwa gharama ya £ 34 milioni, na kumfanya kuwa mchezaji wa gharama kubwa zaidi wakiafrika na kuanza safari mpya. Alicheza michezo 27 na mmoja akitokea bench na kuwania nyavu mara 13 kwa msimu huo.

Sasa sadio Mane ni mtambulisho mkubwa wa nchi yake ya Senegal. Mané amepata kucheza zaidi ya 40 kwa Senegal tangu mwanzo mwaka 2012, na aliwakilisha timu ya kitaifa katika Olimpiki za 2012, 2015 Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Mataifa ya 2017.Bado anasafari ndefu na ngumu yakuipatia nchi yake kikombe cha mataifa ya afrika, sii hapo tuuh. Hata majogoo wa jiji wanakiu ya kukinyenyua kikombe cha klabu bingwa ulaya.

Leave a Comment