Ligi Kuu Tanzania Bara: Yanga Sc yavunja mwiko, Tanzania Prisons ya watambia mahasimu zao

Ligi Kuu Tanzania Bara: Yanga Sc yavunja mwiko, Tanzania Prisons ya watambia mahasimu zao

Yanga Sc imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Yanga hakuwahi kuibuka na ushindi kwenye uwanja wa CCM Kirumba thidi ya Mbao pia haikuwa kufunga goli thidi ya team hiyo , Makambo amekuwa mchezaji wa kwanza kupachika bao na mwinyi zahera amekuwa kocha wa kwanza kuifunga Mbao FC

Kwa ujumla katika Ligi Kuu, timu hizo zimekutana mara tano na Yanga imeshinda mechi nne huku machi tatu zikiwa ni Dar es Salaam, wakati Mbao wameshinda mechi mbili zilizopita za Mwanza.

Robert Ndaki alianza kuifungia Mbao FC kwa kichwa dakika ya 45 akimalizia krosi ya Amos Charles kutoka upande wa kushoto huku mshambuliaji Heritier Ebenezer Makambo akaisawazishia Yanga dakika ya 50 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Papy Kabamba Tshishimbi, wote wa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe akaifungia Yanga bao la ushindi kwa penalti dakika ya 68 baada ya beki Erick Muliro wa Mbao FC kuunawa mpira uliopigwa na Kelvin Yondan kwenye boksi.

Ushindi unazidi kuwafanya Yanga SC waendelee kuongoza Ligi Kuu, sasa wakifikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 25, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 50 za mechi 24 na mabingwa watetezi Simba SC ni wa tatu kwa pointi zao 42 za mechi 17.

Kwenye mchezo mwingine bao la Salum Kimenya dakika ya 70, limeipa Tanzania Prisons ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Mbeya City katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 27, ikijiinua hadi nafasi ya 12 kutoka ya 17, wakati Mbeya City inayobaki na pointi zake 30 baada ya kucheza mechi 25, inashuka kwa nafasi moja hadi ya 15.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Sadallah Lipangile dakika ya pili tu limeipa ushindi wa 1-0 KMC dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. KMC inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 27

Ndanda SC imeichapa Singida United 2-0 mabao ya Vitalis Mayanga dakika ya tisa na Mohamed Mkopi dakika ya 81 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Ndanda FC inajiinua hadi nafasi ya 13 kutoka ya 18 ikifikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 26, wakati Singida United inayobaki na pointi zake 29 katika mechi ya 25, inashuka kwa nafasi mbili hadi ya 18.

Stand United imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Mabao ya Stand United yamefungwa na Mourice Mahela dakika ya 33, Datus Peter dakika ya 59 na Nahodha Jacob Masawe dakika ya 90 na ushei, wakati ya Lipuli FC yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 28 na Jimmy Shoji dakika ya 72.

Kwa ushindi huo, Stand United inapanda hadi nafasi ya 10 kutoka ya 14, ikifikisha pointi 33 katika mechi ya 28, wakati Lipuli FC inashuka kwa nafasi moja hadi ya tano, ikibaki na pointi zake 38 baada ya kucheza mechi 27.

Leave a Comment