Ligi Kuu Tanzania Bara: Simba ya endeleza wimbi la ushindi , Azam yaambulia sare

Ligi Kuu Tanzania Bara: Simba ya endeleza wimbi la ushindi , Azam yaambulia sare

Simba Sc imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha

Simba SC iliyochini ya kocha Mbelgiji Patrick Aussems inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 17 ikiendelea kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Azam FC yenye pointi 50 za mechi 24 na Yanga inayoongoza kwa pointi zake 58 baada ya kucheza mechi 23.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na washambuliaji, Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga mawili, moja kila kipindi na linguine Adam Salamba.

Bocco aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya 28 baada ya Emmanuel Semwanza kuunawa mpira uliopigwa na Pascal Wawa kutoka upande wa kulia, baaaye Adam Salamba akaifungia Simba SC bao la pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa Douglas Kisembo kufuatia shuti la Nahodha, John Raphael Bocco, Dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili Bocco akaifungia Simba SC bao la tatu akimalizia krosi nzuri ya kiungo chipukizi Rashid Juma kutoka upande wa kushoto.

Baada ya bao hilo, African Lyon ikamtoa kipa Douglas Kisembo na nafasi yake kuchukuliwa na Tony Charles aliyekwenda kumalizia vizuri mchezo kwa kutoruhusu mabao zaidi.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Coastal Union walitangulia kwa bao la Ayoub Lyanga dakika ya 45 na ushei kabla ya Obrey Chirwa kuisawazishia Azam FC dakika ya 51.

Mwadui FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya jirani zao, Biashara United ya Mara Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga, mabao yote ya Mwadui FC yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Salim Aiyee dakika ya 45 na 64, wakati la Biashara United limefungwa na Waziri Junior kwa penalti dakika ya 50.

Leave a Comment