Kylian Mbappe aongoza jahazi kwenye uwanja wa Old Trafford.

Kylian Mbappe aongoza jahazi kwenye uwanja wa Old Trafford.

Manchester United lazima wafanye kazi ya ziada kufufua ndoto ya kusonga mbele baada ya kufungwa mabao 2- 0 na Paris St-Germain katika uwanja wa Old Trafford.

Mabao ya Presnel Kimpembe na Kylian Mbappe yaliwapatia ushindi mabingwa wa Ufaransa. Ushindi wa mara 10 wa United katika mechi 11 chini ya meneja wao wa muda Ole Gunnar Solskjaer ulifufua matumaini yao ya kuwa tena mabingwa wa ulaya.

Matumaini ya Solskjaer yalididimizwa na majeruhi ya Jesse Lingard na Anthony Martial katika kipindi cha kwanza lakini PSG waliimarisha mashambulizi yao bila uwepo kwa wachezaji nyota wao Neymar na Edinson Cavani.

Kitumbua cha United kiliingia mchanga zaidi, baada ya Paul Pogba kutupwa nje dakika ya mwisho ya muda wa ziada alipolishwa kadi ya njano mara ya pili katika hatua ambayo itamkosesha mechi ya marudio.

Solskjaer amefanya kazi ya kuwatia motisha wachezaji baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi mwezi Disemba - lakini usiku wa Jumanne ya Februari 12 ulikuwa mrefu kwake tangu alipotua Old Trafford

Angel Di Maria ameandikisha rekodi ya kuchangia ufungaji mabao katika Champions League kwa mara ya tatu, na ya kwanza tangu mwezi Septemba 2013 (wakati wa mechi ya Real Madrid dhidi ya Galatasaray).

Gianluigi Buffon amekuwa mchezaji wa nne kucheza Champions League akiwa na mika 41 (baada ya Marco Ballotta, Mark Schwarzer na Oleksandr Shovkovskiy); Alishiriki mashaindano hayo mra ya kwanza kabla ya wachezaji Marcus Rashford na Kylian Mbappe kuzaliwa.

Kwanzia mwanzo wa msimu wa mwaka 2016-17, ni Cristiano Ronaldo pekee aliyefunga mabao mengi zaidi (mabao16) katika mechi za muondoano za Champions league kuliko Kylian Mbappe wa PSG aliyefunga (mabao 7) kufikia sasa.

Leave a Comment