Kilichojiri Deadline day: Cahill, Malcom, Hudson-Odoi, Janssen, Austin

Kilichojiri Deadline day: Cahill, Malcom, Hudson-Odoi, Janssen, Austin

Dirisha dogo la Usajili la Mwezi januari limefungwa kwa baadhi ya nchini huku nyota kadhaa wakisajiliwa katika vilabu mbalimbali barani ulaya

Burnley wamesajili Peter Crouch ambae mkataba wake utadumu mpaka mwisho wa msimu, Mshambuliaji huyo alifikisha miaka 38 jumatano tano iliyopita na anakuwa amechezea jumla ya vilabu sita ya Epl.

Mshambuliaji wa Liverpool Lazar Markovic amejiunga na klabu ya Fulham bure, huku mshambuliaji wa klabu hiyo ya Fulham Aboubakar Kamara akijiunga na waturuki wa Yeni Malatyaspor.

Wajerumani wa Borussia Dortmund wamemtoa kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu, kiungo wake Shinji Kagawa kwenda kujiunga na watukutu wa Kituruki Besiktas.

Leicester City , wao wamemsajili kwa mkopo kiungo toka Monaco,Youri Tielemans huku Monaco wakimchukua Adrien Silva kutokea kwa vija hao wa viunga vya King Power.

Mlinzi wa Chelsea raia wa England Gary Cahill, 33, amekataa ofa za dakika ya mwisho kujiunga na klabu za Juventus, Monaco na Fulham. (Sky Sports)

Bayern Munich wametupilia mbali mipango ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18, baada ya kutangaza kuwa hawatawasaini wachezaji wengine zaidi msimu huu. (Goal)

Eddie Nketiah atasalia katika uwanja wa Emirates baada ya uhamisho wake kuenda Augsburg kwa mkopo kugonga mwamba. (Football.London)

Mazungumzo kati ya Schalke na Tottenham kumhusu mshambuliaji wa Uholanzi Vincent Janssen, 24 yamegonga mwamba. (Football.London)

Southampton wamekataa ofa ya vilabu vinne vya ligi kuu ya England ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wake Charlie Austin, 29. (Sky Sports)

Udinese wameachana na azma yao ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Derby,Tom Huddlestone, 32. (Derby Telegraph)

Leave a Comment