Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Yaunguruma

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Yaunguruma

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia Katibu Mkuu wa Rhino Rangers, Dickson Mgalike kutojihusisha na soka kwa miezi mitatu na kumtoza faini ya Sh. Milioni 1 kwa tuhuma za kuongoza mashabiki wa timu yake kuwapiga marefa na Kamisaa. Mgalike anadaiwa kufanya kosa hilo baada ya mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara dhidi ya Arusha United uliofanyika Februari 2, mwaka huu Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na ameadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 29 (9) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba katika kikao chake Februari 9, mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Kiomoni Kibamba, Kamati pia imeipiga faini ya Sh. 500,000 Rhino Rangers kutokana na vurugu hizo. Ndimbo amesema Rhino Rangers inatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku 30 kwa kuzingatia Ibara ya 15(3) ya Kanuni za Nidhamu za TFF.

Mmiliki wa Changanyikeni Rangers FC, Omary Bawazir amepewa Onyo Kali kwa mujibu wa Ibara ya 10(a) ya Kanuni za Nidhamu za TFF baada ya kukiri kuingia uwanjani katika eneo la kuchezea (pitch) wakati wa mechi dhidi ya Cosmopolitan iliyochezwa Februari 2, 2019 Uwanja wa Chuo cha Bandari, Dar es Salaam.

Kamati imekazia faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa Changanyikeni Rangers FC iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72), na kuwa faini hiyo ilipwe ndani ya siku 30.

Kiongozi wa Arusha FC, Hassan Issa amepewa Onyo na kutozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kutiwa hatiani kwa kutaka kumpiga Mwamuzi katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Arusha United SC iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

Dennis Shemtoi ambaye pia ni Kiongozi wa Arusha FC naye amepewa Onyo na kutozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kutiwa hatiani kwa kutaka kumpiga Mwamuzi katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Arusha United SC

Kiongozi wa Arusha FC, Bw. Amasha Masenga amepewa Onyo na faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Ibara za 10(a) na 15(2) za Kanuni za Nidhamu za TFF.

Meneja wa Kumuyange FC, Josephat Sinzo amepewa adhabu ya Onyo na faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Ibara za 10(a) na 15(2) za Kanuni za Nidhamu za TFF

Mchezaji Dastani D Lipinga wa Mgambo Shooting amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 38(7) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mchezaji Rashid A Shilla wa Mgambo Shooting amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 38(7) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mtunza Vifaa (Kit Man) Alimu Hadji wa Mashujaa FC amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Daktari Adamu Maftar wa Mashujaa FC amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Meneja wa Transit Camp, Bw. Moshi Hamisy amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi sita (6) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza

Kocha Msaidizi wa Transit Camp, Thomas Gama amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Kiongozi wa Transit Camp, Santos Kato amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2)ya Ligi Daraja la Kwanza.

Leave a Comment