Gonzalo Higuain aanza kwa mkosi ligi kuu Wingereza (EPL)

Gonzalo Higuain aanza kwa mkosi ligi kuu Wingereza (EPL)

Gonzalo Higuain mchezo wake wa kwanza wa ligi akiwa na kikosi cha Chelsea waki pokea kipigo kizito cha goli nne bila majibu kutoka kwa klabu ya Bournemouth , Higuain alitumikia mchezo dakika 65 tu na nafasi yake kuchukuliwa na Olivier Jonathan Giroud , Maurizio Sarri akikiri mchezaji wake alikuwa hayupo kwenye utimamu mzuri wa mwili huku ikisadikika kuwa na tatizo la nyuma ya mgongo .

Kipigo hicho ni kikubwa zaidi kwa Chelsea kwa kipindi cha miaka 23 kwenye Ligi ya Premia. Kipigo kikubwa cha ‘mbwa koko’ ambacho Chelsea ilipokea ilikuwa Septemba 1996 walipofungwa 5-1 dhidi ya Liverpool.

Gharika langoni mwa Chelsea ilianza dakika mbili tu baada ya mapumziko kwa Joshua King kuandika goli la kwanza katitika dakika ya 47, King alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Chelsea kwa kutengeneza goli la pili lililofungwa na David Brooks katika dakika ya 63. Goli la tatu lilifungwa na King katika dakika ya 74 kabla ya Charlie Daniels kupigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Chelsea katika dakika za majeruhi (90+5).

Kipigo hicho kimewashusha Chelsea mpaka nafasi ya tano wakiwa sawa na Arsenal kwa alama 47 lakini Gunners wapo nafasi ya nne kwa kuwa wamefunga magoli mengi kuliko Blues, Chelsea walianza msimu kwa kutofungwa katika michezo 12 lakini sasa wameshapoteza michezo minne kati ya 12 waliyocheza hivi karibuni.

Ushindi wa Bournemouth unaifaya klabu hiyo kupaa mpaka nafasi ya 10 kwenye msimao wa ligi na kufikisha alama 33.

Leave a Comment