breaking news New
Hassan Kessy azidi kupeperusha bendera

Hassan Kessy azidi kupeperusha bendera

Kwenye mchezo wa Charity Shield Ngao ya hisani ambao pia huwa unatumika kama sehemu ya ufunguzi wa ligi ya Zambia ulichezwa baina ya Zesco vs Nkana. Mpaka dakika tisini zinakamika jana.

Zesco 1-1 Nkana.

Nkana walitwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Nkana. Hassan Kessy bado anapeperusha Bendera ya Tanzania. Kwa mara nyingine tena anabeba kombe la 2 kwenye msimu wake wa kwanza.

Katibu wa shirikisho la COSAFA Sue Destombes amekutana na viongozi wa soka kutoka Zimbabwe na kuwamwagia sifa kedekede.

Sue ametoa mawazo yake kuwa hali ya miundo mbinu ya soka nchini humo inatoa ishara njema kuwa mashindano ya COSAFA yafanyike huko. Amesema kuwa anatumai mashindano hayo yaatanza nchini humo kuanzia tarehe 19 mwezi Mei.

Zimbabwe iliandaa mashindano hayo mara ya mwisho mwaka 2009, na baadae 2011 na 2017 wakaandaa michuano ya wanawake.

Kocha mkuu wa Nigeria Rohr amesema haona nafasi kwa wachezaji wa ndani kupata nafasi kwenye kikosi chake.

“ninvigum sana kupata wachezaj wa ligi ya ndani kupata nafasi kwa sababu wengi wamekaa muda bila kucheza” Rohr

Ikumbukwe msimu uliopita ligi kuu Nigeria ilisimama ikiwa mzunguko wa 24 baada ya matatizo ya kiutawala. Ilipofika mwezi wa 8 mwaka jana ligi ilisimama na hakuna bingwa aliyetawazwa wala waliokuwa mwishoni mwa ligi hawakushuka daraja.

Leave a Comment