Fenway Sports Group waimba wimbo wa Liverpool kwa mara ya kwanza.

Fenway Sports Group waimba wimbo wa Liverpool kwa mara ya kwanza.

Kama kuna mtu anaweza kuwa na furaha Zaidi kwenye mafanikio ya Liverpool ni Martin Broughton mbali ya kuwa shabiki wa kutupwa wa Chelsea, Mafanikio ya Liverpool yameanzia kwenye nguvu na ujasiri wake wa kupigana kuwaondoa Tom Hicks and George Gillett walioangalia pesa zaidi bila ya kujali hisia za mashabiki , mbali ya uwekezaji wa kukurupuka wa Hicks and Gillett wa kumwajiri mwalimu mkongwe Roy Hodgson na usajili wa mafungu Milan Jovanović , Joe Cole, Christian Poulsen, Raul Meireles, Paul Konchesky haukuleta tija kwenye team na haikuzuia team kupokwa kwenye mikono yao na Maisha ya Martin Broughton hayakuwa marefu Liverpool na nafasi yale kushikwa na Tom Werner .

Tom Werner alitumia malengo ya New England Sports Ventures kipindi hicho kwa sasa ikijulikana kama Fenway Sports Group, LLC (FSG) na kuanza na uwekezaji wa mbinu nakuleta hamasa mpya kwa mashabiki waliokata tamaa, haikushangaza wengi kuona mwalimu mkongwe Roy Hodgson akipokwa ajira yake na legend wa club Sir Kenneth Mathieson Dalglish kukabiziwa team kwa sifa mbili kubwa ilitambulika ataleta hamasa kwa mashabiki na kuleta mbinu mbadala , mbali ya mwanzo mzuri wa Dalglish hakuweza kuvumilika machoni kwa Tom Werner na kumpoka ajira ,mbali ya kukashifiwa na wengi akiwemo wachambuzi wakubwa mfano ni Alan Hansen .

Fenway Sports Group, LLC (FSG) waka mwamini Brendan Rodgers, msimu wa kwanza haukuwa mzuri sana kwa Rodgers mbali ya kumaliza nafasi moja juu (7th) ya msimu uliopita chini ya Dalglish , msimu wa 2013–14 ulikuwa ni wafuraha na majozi makubwa kwa mashabiki na uwongozi kwa ujumla, Liverpool wakiwa point 5 mbele ya man city huku zikibaki match tatu kumaliza msimu , kipigo cha Anfield kutoka kwa Chelsea kilitoa tumaini kwa bingwa Man city .

Suluhu thidi ya Crystal Palace iliwamwaga machozi wengi achia mbali kilio cha Luis Suarez kilicho tafsiri safari yake ya Barcelona, zikiwa zimebaki dakika 11 mpira kwisha
matokeo yakiwa 3-0 liverpool wakiongoza, mambo yakabadilika gafla na kuambulia suluhu ya bao 3-3 nakuondoa matumaini ya ubingwa wa kihistoria , moja ya kumbukumbu kubwa ni kuvunjwa kwa record ya club ya msimu wa 1895–96 idadi kubwa ya mabao kufungwa kwa msimu moja mabao 101, Liverpool walirudi kwenye mashindano ya UEFA Champions league baada ya miaka mitano kuikosa,

Upande wa pili Rodgers hakutoka patupu aliondoka na tuzo ya heshima ya LMA Manager of the Year Award nakuweka record ya club kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20, kwa sasa tuzo hii ipo mikononi mwa Christopher John Wilder baada ya kusaidia kuipandisha Sheffield United, Nyota ya Rodgers ilizidi kufifia kwa misimu iliyoendelea na kuweka record ya kuwa manager wa kwanza kushinda kushinda kikombe kwenye misimu 3 ya mwanzo na kuambatana na vipigo vya kihistoria kama cha mabao 6-1 kutoka kwa Stoke city na ndoto ya kuirudisha Liverpool kwenye michuano ya ulaya ilipotea kwenye imaya yake hakuvumilika mbele ya Tom Werner kwenye kivuli cha Fenway Sports Group, LLC (FSG).

Fenway Sports Group, LLC (FSG) wakaunda project mpya chini ya mjerumani Jürgen Norbert Klopp ambaye aliamini anaweza kufanya kazi ngumu iliyoshindwa na wengi hapo nyuma akipewa objective za team kuwa EPL kipaumbele na Mashindano ya Ulaya ni tamadunia ya Club, hawakusita kumpa muda na kiasi alichotaka kwenye uwekezaji , Klopp
amefanikiwa kurudisha club kwenye ushindani na kutimiza ahadi moja ya ubingwa wa ulaya kama tamaduni ya club ,huku akibakiza deni la ubingwa wa uwingereza ambao ni fumbo kubwa kwa sasa .

Leave a Comment