breaking news New
Denis Suarez kutatua tatizo la ubunifu wa Arsenal

Denis Suarez kutatua tatizo la ubunifu wa Arsenal

Arsenal imekuwa ikimiliki mpira kwa asilimia kubwa kwenye michezo yake ya karibuni na baadhi wanafika asilimia 70% ya umilki wa mpira, Changamoto kubwa ni ukosefu wa ubunifu huku wengi wakililia huduma ya Mesut Özil ambayo imeshindwa kuonekana kwenye mguu wa Alex Iwobi .

kwa mujibu wa kumbukumbu za Opta Arsenal imeshuka kenye kwenye upigaji wa mashuti yanayolenga goli wa kiwa na wastani wa 12.7 kwa msimu huu wa 2018/19 huku msimu wa 2017/18 wakiwa na wastani wa 15.6, msimu wa 2008/9 na 2009/10 ukiwa ndio msimu bora wastani wa 17.4, changamoto ya ubunifu wa kwenye tatu ya mwisho ya uwanja ipo nyuma kwenye kumbukumbu wastani wa 51.5 pass kwa kila mchezo .

Tatwimu za Arsenal kwenye pass za tatu ya mwisho ya uwanja
Tatwimu za Arsenal kwenye pass za tatu ya mwisho ya uwanja

Msimu wa 2017/18, Suarez alitengeneza wastani wa nafasi 2.2 kwa kila dakika 90 za mchezo huko La Liga akiwa nyuma ya Lionel Messi (2.6) na Ousmane Dembele (2.7) ndani ya Barcelona kwa takwimu hizo hakuna mchezaji wa Arsenal aliyefika kwenye kiwango hicho ya ubunifu msimu huu. mbali ya hapo Suarez alifanya wastani wa dribbles 3.2 kwa dakika 90 za kila mchezo wa la Liga, Lionel Messi (5.6) na Ousmane Dembele (3.9) wakiwa na wastani bora zaidi ndani ya Barcelona.

Picha ikionesha Ubunifu wa Suarez
Picha ikionesha Ubunifu wa Suarez

Leave a Comment