breaking news New
Chile yaanza kampeni za kutetea Taji

Chile yaanza kampeni za kutetea Taji

Yafuatayo ni mambo tuliyoyaona katika mchezo huo kwa uchache…...

1.Charles Aranguiz ndiye mchezaji bora wa mchezo Katika mchezo dhidi ya Japan Aranguiz amefanikiwa kutoa pasi 2 za magoli ,Key Pasi 7.Uwezo wake mkubwa ni katika kupiga pasi ndefu ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa na madhara kwa wapinzani. Aranguiz ndiye aliyekuwa anaipa uwiano Sawa timu ya Chile katika kukaba na kufanya mashambulizi akitumia zaidi mipira ya juu kabla na hata baada ya kutoka kwa Artulo Vidal. Kwangu Mimi huyu ndiye mchezaji bora wa mchezo.

2.Alexis Sanchez anahitaji kurejesha imani na hali akiwa ndani ya uwanja. Katika kipindi cha kwanza Sanchez hakuonekana kuwa na athari zozote huku akipoteza nafasi 2 za kufunga. Imani imekosekana kwa Sanchez kutokana na kukosa muda wa Mara kwa Mara Wa kucheza akiwa na klabu yake ya Manchester United. Goli moja na assist 1 katika mchezo dhidi ya Japan kuna uwezekano ikamsaidia Sanchez katika kurejesha hali ya kujiamini ndani ya uwanja.Copa America ni sehemu sahihi ya Sanchez kurejesha hali ya kujiamini.

3.Kualikwa kwa Japan katika mashindano haya kunaweza kuwa na faida kwao kutokana na kupangwa na timu zenye uwezo mkubwa wa kusakata soka ,Chile na Uruguay ni kipimo kizuri kwao.

©Timotheo S John

Leave a Comment