Bostwana FA ya vunja mkataba wa David Bright

Bostwana FA ya vunja mkataba wa David Bright

Chama cha Soka Botswana (BFA) ya tangaza kumfunguliwa njia kocha wa timu ya kitaifa David Bright kufuatia mwenendo wa timu na matokeo yasiyothibitisha.

Katibu mkuu wa BFA Mfolo Mfolo katika mkutano wa waandishi wa habari Jumatano alisema: “tumemfunguliwa njia na kuvunja mkataba kwa maslai ya timu na kocha pia. Tulimpa nafasi ya kuboresha kikosi na team kuliweka taifa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa soka duniani (FIFA Rankings) walau kwa nafasi 15 kusogea juu na hatukufanikiwa pia tumekosa sifa kwenda AFCON 2019 “.

Botswana (Zebra) sasa ipo nafasi 145 katika msimamo wa soka la dunia (FIFA Rankings), imeshuka nafasi 24 kutoka 121 Julai 2017 wakati Bright anachaguliwa kuwa mkufunzi mkuu wa timu hiyo , pia wameshindwa kupata ushindi kwenye mechi tano za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya 2019 Afrika.

Mfolo alieleza kwamba kutokana na utendaji na mwenendo wa timu ya kitaifa “ilikuwa busara kuvunja mkataba na kocha David Bright, BFA inatarajia hivi karibuni kuteua timu ya kiufundi ya mpito ambayo itasaidia kuandaa Botswana (Zebra) kwa mchezo wao wa mwisho wa kufuzu kwa AFCON dhidi ya Angola mwezi ujao.

Leave a Comment