Azam yaduwazwa Mbeya, Biashara United walamba sukari

Azam yaduwazwa Mbeya, Biashara United walamba sukari

TIMU ya Azam FC leo imekamilisha mechi tatu bila ushindi baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Tanania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Jumanne Elfadhili aliyemchambua kipa Benedict Haule kwa mkwaju wa penalti dakika ya 36 baada ya beki wa Azam FC, Mghana Yakubu Mohamed kuunawa mpira uliopigwa na Ezekia Mwashilimbi. Azam FC inabaki na pointi zake 48 baada ya kucheza mechi 22, ikiendelea kuzidiwa pointi tisa na vinara,

Tangu January 2019, Tanzania Prisons imepoteza mchezo mmoja tu (January 2, 2019-Lipuli 1-0 Tanzania Prisons) baada ya hapo wamecheza mechi 8 mfululizo bila kupoteza. Wametoka sare katika mechi mbili na kushinda michezo mitano ya ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo mwingine timuya Biashara United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

Mabao ya Biashara United leo yamefungwa na George Makang’a dakika ya 39 na Innocent Edwin dakika ya 80, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na mtokea benchi Riphat Khamis dakika ya 64. Kwa ushindi huo, Biashara United inayofundishwa na beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Amri Said ‘Stam’ inafikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi 27 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, ikiishushia mkiani African Lyon yenye pointi 20 za mechi 24.

Mtibwa Sugar, mabingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo 1999 na 2000 inabaki na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 23, ikiendelea kukamata nafasi ya 11.
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, bao pekee la Jumanne Elfadhili dakika ya 36 limeipa Tanzania Prisons ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga mabao yake yakifungwa na Wallece Kiango dakika ya 65 na Salim Aiyee dakika ya 79 dhidi ya lile la Ayoub Lyanga dakika ya 75.

Leave a Comment